WAKATI mashabiki wa Simba wakiicheka na kuibeza Yanga kwa kulazimishwa sare na Lipuli, rekodi zinaonyesha kuwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara bado wanaweza kuwafunika watani zao na kutwaa taji.

Simba iliifunga Ruvu Shooting mabao 7-0 katika mechi ya ufunguzi wa Ligi wakati Yanga ilikwama nyumbani licha ya kucheza na timu iliyopanda daraja tu.

Hata hivyo rekodi zinaonyesha katika kipindi cha miaka saba iliyopita, Yanga imekuwa ikianza ligi vibaya, lakini hutwaa ubingwa.

Katika kipindi hicho, haikushinda katika mechi tatu za ufunguzi, lakini ni mara moja tu ndio haikutwa taji.

Comments

0