LIGI Kuu Bara imeanza, lakini itakwenda mapumziko ikiwa zimechezwa mechi nane tu za raundi ya kwanza. Ligi itasimama kwa muda kupisha pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ dhidi ya Botswana, Zebras.

Mechi hiyo itachezwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa imo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Inakanganya kidogo ukiipitia ratiba iliyotolewa mapema na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inaonyesha kuwa shirikisho hilo lilikuwa linafahamu wazi kuwa, kati ya Agosti 28 mpaka Septemba 5 ni wiki ya michezo ya kirafiki ya kimataifa inayotambuliwa na Fifa, lakini Bodi ya Ligi (TPLB) ilipanga mechi za Ligi Kuu ndani ya wiki hiyo.

Comments

0