MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc,  kwenye uwanja wa Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club, kitarejea  Dar es Salaam siku ya jumatatu, tayari kwa kukwea ‘pipa’ jumanne alfajiri kueleka Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya wenyeji Mwadui Fc uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Kambarage.

Akizungumza na  www.yangasc.co.tz  Ofisa habari wa kikosi hicho cha mabingwa wa soka wa kistoria nchini, Dismas Ten  ameweka wazi kuwa matayarisho yote kwa ajili ya safari hiyo yanakwenda vizuri, na kinachosubiriwa sasa  ni wakati tu kuweza kufanya safari hiyo.

Kama ambavyo unafahamu, jumapili timu yetu itakuwa Lindi kwenye uwanja wa Majaliwa, kucheza mchezo wa kirafiki na Namungo Fc, baada ya mchezo huo tunatarajia kikosi kitarejea Dar siku ya  jumatatu asubuhi na jumanne alfajiri itasafiri kwenda Shinyanga, kwa ajili ya mchezo wa ligi siku ya alhamisi.

Akiendelea  zaidi Ten alisema kuwa, wanafahamu ubora wa Mwadui Fc ikiwa inacheza uwanja wa Kambarage, hivyo Yanga ina kila sababu ya kujiandaa vyema ili kuweza kupata matokeo kwenye mchezo huo utakaochezwa alhamisi  jioni kwenye uwanja wa Kambarage.

Mwadui ni timu nzuri wamekuwa wakipata matokeo wanapocheza nyumbani, tunafamu hilo ndiyo sababu tumefanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki kwa ajili ya kupima uwezo wetu, imani ya kila mmoja klabuni kwentu ni kuwa tunakwenda kupambana ili tupate matokeo mazuri.

Katika hatua nyingine Ten amedokeza kuwa kocha mkuu Zahera Mwinyi anatarajia kutua nchini siku ya jumatatu jioni akitokea Congo DRC tayari kujumuika na benchi lake la ufundi kwa ajili ya safari ya Shinyanga.

Mwalimu alikuwa Congo DRC kwenye majukumu ya timu ya taifa, atarejea nchini jumatatu jioni kwa ajili ya safari, hakuna shaka yoyote juu yake kwa  wote tunafahamu juu ya majukumu aliyonayo kwenye taifa lake lakini pia umuhimu mkubwa alionao na anaoutoa kwa timu yetu.

Juma Mahadhi, ameanza mazoezi mepesi baada ya kukosekana dimbani muda mrefu kupisha upasuaji mdogo wa goti aliofanyiwa.

Comments

2
Abou Salimu 9:18 pm November 16, 2018

Congs Yanga

Jaclyn 6:52 am January 18, 2019

I thuhogt finding this would be so arduous but it’s a breeze!