MKUU wa kitengo cha utabibu kikosini, Dr Edward Bavu amethibisha kuwa ni wachezaji wanne pekee ambao bado ni majeruhi kwa sasa kutoka idadi ya wachezaji 11 waliokuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu wakiuguza majeraha waliyopata kwenye michezo mbalimbali  ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Akizungumza muda mfupi uliopita mara baada ya kumalizika kwa mazoezi asubuhi ya leo kwenye viwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaa, Dr Bavu amesema kuwa  limekuwa jambo jema kwa benchi la ufundi na wanachama na mashabiki wa Yanga kurejea kikosini kwa nyota saba  ambao hawakutumika kwenye michezo iliyopita licha ya umuhimu wao katika kikosi cha kwanza.

Tulikuwa nje ya furaha,kuwakosa wachezaji zaidi ya 10 kwenye kikosi  ni wazi huwezi kuwa sawa, jambo jema ni kuwa saba kati yao tayari wameanza mazoezi ni wanne tu kwa sasa ambao watalazimika kusubiri mpaka baadae kujua hatima yao.

Akiendelea  zaidi Dr Bavu aliwataja wachezaji wote ambao wamepona kutoka majeraha na wako tayari kurejea uwanjani kuanza tena. kutimiza majukumu yao baada ya kuwa nje kw  majuma kadhaa.

Rostand,Juma Abdul,Hadji Mwinyi, Andrew Vicent,Pato Ngonyani,Thabani Kamusoko,Ibrahim Ajib wote hawa wako tayari kwa kurejea. uwanjani, hii ina maana kuwa wataalamu wetu wa ufundi wanaweza kuwatumia endapo wataoana inafaa kufanya hivyo kulingana na mazoezi waliyowapa, wakati mwingine mchezaji kucheza inahitaji utimamu wa asilimia mia moja.

 

Comments

27
Ally Mwalasha 3:43 pm February 9, 2018

Hyo ni habari njema kwetu….DAIMA MBELE NYUMA MWIKO

amzasaid 4:27 pm February 9, 2018

Itapendezasana kamakamusokoatacheza kesho

oganga 4:34 pm February 9, 2018

safi sana,tukutane kesho taifa…..daima mbele nyuma mwiko

Remmy Urio 5:18 pm February 9, 2018

Tunashukuru kwa taarifa hizo, ni habari njema kwetu wapenzi.

Mark Ringia 5:34 pm February 9, 2018

Kazi nzuri, Hongera Dismas…..

Mark Ringia 5:34 pm February 9, 2018

Kazi nzuri, Hongera Dismas…..

Albert Mringo 5:50 pm February 9, 2018

safiiiii daima mbeleeee mwiko kurud nyumaaaa

Salimuabou 6:08 pm February 9, 2018

Afadhali bunduki zimerejea…

Tumaini Elias 6:49 pm February 9, 2018

Message… *safi sana

Lawn 8:13 pm February 9, 2018

Ni habari njema kwa ustawi wa kikosi chetu katika mashindano yaliyopo mbele yetu pamoja na kujiweka sawia katika kutetea ubingwa wa VPL

Haji ngoteyega 8:30 pm February 9, 2018

Safi sana hiyo

Frank Mwalongo 8:30 pm February 9, 2018

Good news!! Let’s go Young Africans

Abarikiwe Mwamonje 9:35 pm February 9, 2018

Habari njema hizi..Yanga timu yangu Yanga taifa langu.DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.

Moumin Mwatawala 9:45 pm February 9, 2018

Tunashukuru na kuwaombea waliobaki wapone haraka na kuja kuitumikia timu. Kwa pamoja tunaweza na kwa pamoja tutashinda. Daima mbeleee??

Jerome Mapile 9:47 pm February 9, 2018

Ni habar njema kwetu

Oyooooooo kesho hiyo 3 tu 10:22 pm February 9, 2018

Oyooooooo kesho hiyo 3 tu

oscar lyimo 10:46 pm February 9, 2018

daima mbele nyuma mwiko

nimekubari kitengo cha habari hakika tumepiga hatua 10:56 pm February 9, 2018

kampa kampa tenaaaaaaaaaaa

Abdul zazaworldwide qamis 10:58 pm February 9, 2018

kamusoko

Edrick Mwinuka 11:02 pm February 9, 2018

Asante. Tuombe Mungu waliobaki wapone mapema na waliopo wasipate tena Majeraha

lawrence mwasenga 11:30 pm February 9, 2018

hakika itapendeza wataalam Ajib na kamsoko, mkomola kurudi

Nzwalah Jr Tz 11:31 pm February 9, 2018

yuko wapi canavaro

Fadhil 11:34 pm February 9, 2018

Kamusoko tunakukumbuka sana

Dmrutu 9:50 am February 10, 2018

habari njema kwa Yanga kwenye michuano ya kimataifa na kuwania taji letu tulilolizzoea, habari mbaya kwa Simba kwani gemu zidi ya Simba Ajib, tshishimbi,kamuso,Chirwa ndani ya Nyumba

McNamara Cogan 5:02 pm February 12, 2018

Tunaendelea kufarijika DAIMA MBELE

Pius John 12:00 am February 13, 2018

Mungu yuko nasi

chocopie 1:09 pm December 21, 2018

6wSdvX Wow, fantastic blog layout! How long have you been blogging for? you make blogging look easy. The overall look of your site is magnificent, let alone the content!. Thanks For Your article about sex.