MABADILIKO yaliyofanywa na kocha George Lwandamina kumtoa Ibrahim Ajib na kumuingiza Juma Mahadhi katika dakika 64 kipindi cha pili yalitosha kuipa Yanga ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wageni St Louis Fc kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya Mabingwa  Afrika.

Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, dakika 45 za kwanza zilimshuhudia Obrey Chirwa akikosa mkwaju penalti baada ya  Hassan Kessy kuagushwa ndani ya eneo la hatari,hivyo kuhitimisha kipidi cha kwanza kilichokuwa na kosa kosa nyingi timu zote zikienda mapumziko zikiwa nguvu sawa.

Mara baada ya mchezo,kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa alisema anawashukuru wachezaji kwa kucheza vizuri na kupata ushindi licha ya matarajio ya kushinda magoli mengi zaidi yaliyokuwepo awali.

Huu ni mpira wa miguu,matokeo ndani ya dakika 90 yanapaswa kuheshimiwa,tulijiandaa kwa ajili ya kupata ushindi mkubwa lakini wapinzani wetu waalikuja na mbinu yao ya kujilinda zaidi,tulibadili mbinu mara kadhaa kujaribu kutafuta ushindi mkubwa lakini haikuwa hivyo,nawapongeza vijana wetu wamejitahidi kadri ya uwezo wao, tunarudi kambini sasa kuanza matayarisho ya mchezo wa pili.

Hassan Kessy (katikati) akijaribu kuwatoka walinzi wa St Louis Fc.

Comments

2
Egidius Mushubirwa 9:18 pm February 11, 2018

Tunawapongeza kwa ushindi na tunawatakia maandalizi mema kuelekea mchezo wa marudiano hapo tar 21.2. Ushindi ni muhimu ili tusonge mbele.

zvodretiluret 10:06 am September 7, 2018

I’ve recently started a site, the information you provide on this web site has helped me tremendously. Thanks for all of your time & work.

http://www.zvodretiluret.com/