WAKATI mikakati ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji Fc kwenye mfululizo wa ligi kuu ya vodacom jumatano hii,kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka jumapili asubuhi kuelekea Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano na mabingwa wa nchi hiyo St Louis.

Katibu Mkuu wa Yanga Sc, Charles Mkwasa,amesema matayarisho ya safari hiyo tayari  yamekwisha kamilika ikiwa ni pamoja na  taratibu za  usafiri kwa wachezaji na viongozi wa benchi  la  ufundi.

Matayarisho yameshafanyika, jumla ya wachezaji 20 na viongozi 10 wakiwemo wanane wa benchi la ufundi,tunafahamu mchezo  utakuwa tarahe  21/2 hivyo tumeona  umuhimu  wa kwenda mapema ili kupata wasaa wa kuzoea mazingira  na kucheza tukiwa hatuna presha ya hali ya hewa.

Kuhusu Mchezo wa Majimaji Mkwasa alisema,kikosi kinatarajia kuingia kambini kesho kwenye hotel ya Zimbo tayari kwa mchezo huo wa kesho kutwa uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Maandalizi yamekamilika,timu inaingia kambini kesho,mchezo huu ni muhimu kwetu na tumeupa uzito kutosha kwa sababu tunahitaj kushinda,Majimaji ni timu nzuri tunajua utakuwa mchezo wenye upinzani wa hali ya juu.

Charles Mkwasa na Dismas Ten kwenye mkutano na waandishi wa habari.

 

Comments

4
Shaban 11:21 pm February 12, 2018

Asante kwa kutujuza

mbuna 8:24 am February 14, 2018

hongerini kwa kazi bora

Ally 1:48 pm February 14, 2018

Kila la kheri chama langu daima mbele nyuma mwiko

zvodretiluret 9:31 pm August 28, 2018

There may be noticeably a bundle to know about this. I assume you made sure good points in options also.

http://www.zvodretiluret.com/