WAKATI  Yanga sc  ikijiandaa kuivaa MajiMaji Fc kwenye mchezo wa ligi ya Vodacom Kesho jumatano kwenye uwanja wa Taifa, mkuu wa kitengo cha  utabibu kikosini Dr Edward Bavu amethibitisha kuwa  nyota wanne pekee ndiyo hawatakuwa sehemu ya mchezo huo wa kesho.

Akizungumza na yangasc.co.tz  muda mfupi uliopita Dr Bavu amesema kuwa, Amissi Tambwe,Yohana Mkomola, Donald Ngoma na Abdallah Shaibu ni wachezaji ambao bado wako kwenye majeraha na watasalia nje kupisha dakika 90 dhidi ya Majimaji hapo kesho.

Ni vigumu kuwatumia,bado wanauguza majeraha, kama klabu tunafanya jitihada kubwa kuhakikisha kuwa wanarejea uwanjani kuanza kucheza, si jambo jema mchezaji kukaa nje muda mrefu, kuna wakati majeraha huamua hii ni kwa sababu mpira wa miguu una matukio mengi  uwanjani, ni wazi tutawakosa mchezo  Majimaji.

Kuhusu kiungo Thabani Kamusoko,Dr Bavu alisema kuwa mchezaji huyo ameshapona majeraha yake na tayari amekwisha anza mazoezi mepesi kwa ajili ya kuweka sawa utimamu wa mwili.

Kucheza mechi ni jambo ambalo linahitaji utimamu wa mwili asilimia moja,jambo jema ni kuwa mchezaji tayari kashaanza mazoezi, hii inamaana kuwa wakati wowote anaweza kurejea  uwanjani.

 

HILI HAPA GOLI LA DONALD NGOMA  DHIDI YA MAJIMAJI FC, SONGEA.

Comments

3
Jordan Nankoko 11:04 pm February 13, 2018

Ni jambo jema kama majeruhi wameanza kurudi uwanjani. Nguvu ya kutetea ubingwa itaongezeka

Mussa Mtepa 1:33 pm February 14, 2018

Pongezi kwenu kwa taarifa

zvodret iluret 10:06 am September 7, 2018

I have recently started a web site, the information you provide on this site has helped me tremendously. Thanks for all of your time & work.

http://www.zvodretiluret.com/