KATIBU Mkuu wa Young Africans  Sports Club Charles Boniface Mkwasa ametangaza siku maalumu ambayo klabu  itafanya mkutano mkuu wa wanachama wote,kujadili masuala mbalimbali muhimu ya maendeleo.

Muda mfupi uliopita Mkwasa ameiambia  www.yangasc.co.tz kuwa wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada zao mapema kwa sababu kwenye mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.

Mkutano utafanyika Mei 5/2018 hapa jijini Dar es Salaam, wanachama wenye kadi aina zote mbili wataruhusiwa kuingia ukumbuni, kwa maana ya wale wenye kadi za zamani na hizi zinazotolewa sasa kupitia benki ya posta.

Download Hapa

Akiendelea zaidi Mkwasa amesema kuwa, kupitia kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika  jumapili iliyopita, kamati   imeridhia kufanyika kwa Mkutano huo, na kuomba wanachama kujindaa kwa ajenda ambazo zitatangazwa baaadae.

Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga,Dismas Ten, kwenye mkutano na waandishi wa habari, Makao makuu ya klabu.

 

Comments

10
Paul Thomas 1:12 pm March 29, 2018

Thats great news, Viongozi muandae ajenda nzito na muhimu ili zijadiliwe na zifanyiwe maamuzi na mkutano mkuu kwa manufaa ya young Africans, Viongozi mmeonyesha ukomavu mkubwa katika kipindi hiki kigumu cha mpito katika club yetu bila kusahau pongezi kwa mwalimu GL, Technica bench na wachezaji wote kwa kuipambania timu yetu, tumebakiza hatua chache zinazohitaji mshikamano wa hali ya juu kufikia malengo yetu, We still have a chance to achieve, # lets be One, We are One# YASC#EFBN#

Shabani kassanga 1:22 pm March 29, 2018

Tunausubiria kwa ham huo mkutano

Nicholas Mtessa 2:23 pm March 29, 2018

Tunahitaji MABADILIKO YA UENDESHAJI WA KLABU yetu… Mkutano nina imani utakuja na ajenda zilizoshiba kwenye mkutano huo….Yanga si ya kupitisha bakuli kwa wanachama kila uchao…. Hongera Kamati tenddaji kwa kutuletea huo mkutano mkuu

Mohammed J Mzungu 3:02 pm March 29, 2018

Napongeza kamati tendaji kwa kuamua hilo,Yanga inahitaji mabadiliko ya kiundeshaji,hasa ikizingatiwa kwamba mpira wa sasa ni wa kibiashara zaidi,huhitaji mabilioni ya pesa,Bravo…

Kiyungi Twalib 4:12 pm March 29, 2018

Tutafurahi sana kuwepo kwa mkutano huo, maana tunahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye uendeshaji wa timu yetu!

deogratias yinza 4:45 pm March 29, 2018

Hii taarifa za yanga kwa 15501 kwa voda itaanza lini/

fadhil haruna 6:18 pm March 29, 2018

Seriously…… hii kitu niliisubiri kwa hamu kubwa sana,Tunawaomba muandae Agenda zenye kuleta tija kwa yanga,kwani tumepata fundisho kubwa sana katika kipindi hiki kigumu kuwahi kupitia katika club…tunaimani kubwa sana na management kwa ujumla ndio maana tumefika hapa salama……Nawapongeza sana

Damas Kiondo 1:31 am March 30, 2018

Nawatakia Mkutano mwema Wanachama wote wa Yanga

Egidius Mushubirwa 9:47 am March 30, 2018

Tunashukuru kamati ya utendaji kwa uamuzi wa kuwa na mkutano mkuu ili tuweze kuamua mstakabali wa klabu yetu hasa mabadiliko ya uendeshaji.

Andrew Spilu 5:39 pm March 30, 2018

Mungu atafanya mema juu ya huo mkutano