WAKATI  Yanga Sc ikiwa uwanja wa Taifa  kucheza mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika kesho jumamosi dhidi ya St Louis ya shelisheli,imethibitishwa kuwa  waziri wa nchi ofisi ya rais,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mh George Mkuchika ndiyo atakuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.

Muda mfupi uliopita katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ameidokeza www.yangasc.co.tz kuwa  Mh Mkuchika amekubali mwaliko aliopelekewa na klabu ya Yanga kuombwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo namba 25.

Tulimpelekea barua rasmi ya kumuomba kuwa mgeni rasmi, jambo jema ni kuwa amekubali hivyo,nathibitisha rasmi kuwa Mh Mkuchikika ndiyo atakuwa mgeni wa heshima,nichukue nafasi hii kuwa omba wana yanga kuja uwanjani kwa wingi kuungana na Mh Mkuchika katika kuanikiza timu yetu kupata ushindi.

Mh George Mkuchika.

Comments

7
Albert Mringo 5:44 pm February 9, 2018

safii inapendezaaaaaa daima mbele ushindi lazima

Mkombozi Marwa 8:53 pm February 9, 2018

Mungu ibariki Yanga yetu

Rajab 9:39 pm February 9, 2018

Safi sana kwa kuanzia website iko poa tutakua tunaboresha kutokana na challenges zitakazokua zinatokea

Edrick Mwinuka 10:58 pm February 9, 2018

All the best Yanga.

Dr.Mvanda 11:46 pm February 9, 2018

Sawa

Alfred Clement 6:58 am February 10, 2018

Kila la kheri Young Africans, Mabingwa wa Kihistoria!!

Ismail 9:29 am February 10, 2018

Forward ever…Backward Never