MJUMBE  wa kamati ya utendaji ya Yanga Sc, Salum Mkemi amesema mashabiki wa Yanga kamwe hawawezi kuishangilia Simba kwenye mchezo wowote amabao timu hiyo itakuwa. inacheza.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo, Mkemi amesema kuwa. zimekuwepo taaraifa za viongozi wa Simba kuwaomba mashabiki wao kuto kuizomea Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa kesho jambo ambalo haliwafanyi mashabiki wa wa Yanga kuanza kuishangilia Simba.

Hatuwezi kuishangilia Simba,hili halitatokea, tulijaribu mwaka 92 lakini uzalendo ulitushinda, hii ni kwa sababu hatujawahi na hatuwezi kuwa marafiki na wapinzani wetu, kwa hiyo naomba ieleweke wazi kuwa hatuwezi kuishangilia Simba kamwe

Salum Mkemi,Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga sc

Comments

10
Albert Mringo 5:54 pm February 9, 2018

hahahahha namuunga mkono wao waje ila jumapili kuwazomea kama kawaidaaaa

Ambrose Maestro 8:15 pm February 9, 2018

…manara acha kiherehere tuache na Yanga yetu wee vipii

Abdul zazaworldwide qamis 11:20 pm February 9, 2018

yanga raha sana

Filberth 11:27 pm February 9, 2018

Mkemi yupo sawa
All the best our team

G. Hellar 12:54 am February 10, 2018

Yaani tunaanzaje kuishangilia Simba kwa mfano? Big no..

David Chaula 9:38 am February 10, 2018

Najua uhasimu upo, Mimi ni shabiki wa Yanga Sana tu, but hii mentality hasa kwa mechi za kimataifa imetokea wapi? Nina sportsmanship ya kawaida sana Mbona? Najua ni ngumu hasa kwenye Ligi sababu wote ni washindani wa kombe hilo hilo, sasa kwenye mashindano ya kimataifa we are not competitors sasa kutokupeana support kunaanzia wapi?
Kwa hiyo kwa mfano wamekuja MO Bejaia taifa na mashabiki wao halafu zikaanza ngumi kati ya mashabiki wa Morocco na wa Simba tutawapiga mashabiki wa simba ambao by then ni watanzania wenzetu?
Narudia tena mimi ni shabiki wa Yanga Haswaaaaa ila Haji Manara aliongea kiwanamichezo na kizalendo zaidi kuliko alichokiongea Mkemi. Ifike mahali tuwe tunajadili mpira kwa mtazamo mpana na sio uhasimu wa mihemko.
Kwenye Ligi never siwezi kuwashangilia simba labda Kama ushindi wao inanipa faida ya kuwa bingwa nje ya hapo never.

Martin 12:27 pm February 10, 2018

Ni sahihi, kwanza raha ya mpira kuwe na upinzani, sauti mbishano, kwanza watuongeza morali zaidi wakizomea maana tutatia bidii kuwaaibisha.

Hassan 1:05 pm February 10, 2018

Bora uombe mashabiki wa azam wawashangilie sio Yanga…hili jambo haliwezi kutokea. Nahukuru kwa kuliweka wazi jambo hili.

Hassan 1:06 pm February 10, 2018

Bora uombe mashabiki wa azam wawashangilie sio Yanga…hili jambo haliwezi kutokea. Nashukuru kwa kuliweka wazi jambo hili.

zvodretiluret 11:04 am September 7, 2018

F*ckin’ remarkable things here. I’m very happy to see your article. Thanks so much and i am taking a look forward to touch you. Will you please drop me a e-mail?

http://www.zvodretiluret.com/