Baada ya saa 24 za mapumziko kupisha mchezo wa jana  dhidi ya Majimaji uliochezwa uwanja wa taifa na kuhitimisha dakika 90 kwa ushindi mnono wa 4-1,kikosi cha Yanga sc kesho asubuhi kitanaendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho kueleka mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa afrika dhidi ya St Louis ya Shelisheli.

Mapema leo Meneja  wa kikosi  hicho cha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara Hafidh Saleh ameiambia  yangasc.co.tz  kuwa nyota wote wa kikosi cha kwanza watakuwa kwenye uwanja wa Polisi Kurasini kesho asubuhi tayari kwa mazoezi hayo .

Hatutakuwa na wachezaji wanne ambao bado ni majeruhi, Tambwe,Ngoma,Shaibu na Mkomola,jambo zuri ni kuwa Thabani Kamusoko atakuwa sehemu ya wachezaji watakao fanya mazoezi hapo kesho,tunahitaji kufanya matayarisho ya kutosha kabla hatujasafiri kuelekea Shelisheli kwa ajili ya mchezo wa pili na St Louis,tunataka kuwa fit ili tukatafute matokeo  huko huko ugenini.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh (Kushoto) akiwa na Kamusoko kwenye uwanja wa uhuru. (Picha ya maktaba)

Kuhusu tetesi za jina la mlinda mlango Youthe Rostand kuwa halikutumwa kwenye usajili wa Caf,Hafidh amesema kuwa hakuna ukweli wowote kwenye taarifa hizo,jina la golikipa huyo lilitumwa na leseni yake kwa ajili ya kucheza mashindano ya klabu bingwa tunayo.

Ni uzushi tu usiokuwa na maana,jina la Rostand lilitumwa CAF na leseni yake ya  kucheza mashindano tunayo, hivyo siyo kweli kwamba jina lake halikutumwa,kuhusu kucheza au kutokucheza mchezo,siku zote benchi la ufundi ndiyo hupanga kulingana na mipango ya mchezo husika.

Mlinda Mlango namba moja wa Yanga, Youthe Rostand.

 MAGAOLI  MANNE YA YANGA KWENYE MCHEZO DHIDI YA MAJIMAJI HAYA  HAPA…!

Comments

7
Mbelwa 3:05 pm February 15, 2018

SAFI SANA…….DAIMA MBELE NYUMA MWIKO

Ally hassan 3:25 pm February 15, 2018

Waelimishwe wachezaj wetu wakigen hususu slogan kama daima mbele nyuma mwiko ni ya yanga akisema nguvu moja ni ya upande wa pili huyu manyara anapata chakutapika baada ya kuona rostand anaandika yanga nguvu moja

Omary kitale 4:24 pm February 15, 2018

Safi Sana yanga muhimu kujipanga na mechi zijazo

Crispin mathias 8:21 pm February 15, 2018

Kweny Shop registration kila niki weka username naambiwa invalid but cipewi any explanation ya jinsi gan username inatakiwa kuwa , inahusisha character zip.

Naomb msaada katka hilo

mbuna 8:57 pm February 15, 2018

yanga oyeeeeee

Jordan Nankoko 8:53 pm February 16, 2018

Yanga mbele nyuma mwiko

zvodretiluret 10:59 am September 7, 2018

Wow! This can be one particular of the most useful blogs We’ve ever arrive across on this subject. Basically Great. I am also a specialist in this topic so I can understand your hard work.

http://www.zvodretiluret.com/