NYOTA wa kiungo Said Juma Makapu atalazimika kusubiri 90 za mchezo wa Yanga dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda zimalizike kuweza kurudi tena uwanjani kucheza mashindano ya kombe la shirikisho kufuatia adhabu ya kadi mbili za njano alizonazo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Caf, Makapu alipata kadi ya kwanza ya njano kwenye mchezo  dhidi ya Wellayta Dicha kabla ya kupata kadi nyingine kwenye  mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya USM Algers uliochezwa  wiki mbili zilizopitz nchini Algeria.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema ni halala kwa Makapu kupisha dakika 90 za mchezo dhidi ya Rayon kwa sababu ni kweli mchezaji huyo alipata kadi kwenye michezo hiyo iliyotajwa.

Ni kweli alipata kadi kwenye michezo hiyo, muhimu kwa sasa ni benchi la ufundi tayari wanajua  nini watafanya katika kuziba pengo lake  hasa baada ya taaraifa ya Caf kufika klabuni ikisema mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza.

Comments

2
zvodret iluret 9:00 am August 26, 2018

After study a few of the blog posts on your web site now, and I really like your way of blogging. I bookmarked it to my bookmark website record and will likely be checking again soon. Pls try my website online as effectively and let me know what you think.

http://www.zvodretiluret.com/

furtdso linopv 11:37 pm August 31, 2018

I have recently started a web site, the information you offer on this site has helped me greatly. Thank you for all of your time & work.

http://www.furtdsolinopv.com/