KOCHA Zahera Mwinyi anatarajia kusafiri kesho asubuhi kuelekea Morogoro kwa ajili ya kukutana na wachezaji pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi,ili kuzungumza maahache kabla ya kurejea  jijini Dar kukamilisha taratibu za kuanza majukumu yake.

Akizungumza muda mfupi uliopita katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa mapema leo alikutana na Kocha Mwinyi kwa ajili ya kutambuana na kufanya mazungumzo mafupi, na baadae kocha huyo  kuomba kukutana na wachezaji pamoja na viongozi wengine wa benchi la ufundi.

Tumemruhusu kwenda kukutana na timu, apate kujua baadhi ya mambo muhimu kutoka kwa vijana na viongozi wengine wa benchi la ufundi, baada ya hapo atarejea  Dar kuja kukamilisha taratibu za kuanza majukumu ikiwa ni pamoja na mambo ya mikataba, binafsi nafahamu ni kocha mzuri  amekuwa na mafanikio kwenye timu nyingi alizofundisha  na pia amafanya kazi na makocha wakubwa hivyo tunaamini uzoefu alionao unakuja kuleta changamoto mpya kwenya kikosi chetu.

Usikose mahojiano ya kwanza  ya YANGA TV na  kocha Zahera Mwinyi ijumaa hii saa 1:00 usiku kupitia Azamsports2.

Kocha ZAHERA MWINYI.

Comments

2
furtdso linopv 3:59 pm September 6, 2018

Somebody essentially assist to make severely articles I would state. That is the very first time I frequented your website page and up to now? I amazed with the analysis you made to create this particular publish amazing. Excellent activity!

http://www.furtdsolinopv.com/

zvodretiluret 10:41 am September 7, 2018

You have noted very interesting details! ps nice internet site. “Do not quench your inspiration and your inmagination do not become the slave of your model.” by Vincent Van Gogh.

http://www.zvodretiluret.com/