BAADA ya kumaliza dakika 90 za mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison,kikosi cha Yanga kinasafiri leo hii kuelekea Morogoro kuweka kambi kwa ajili ya matayarisho ya mchezo mwingine ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na mchezo wa kimataifa dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda.

Akizungumza na www.yangasc.o.tz  muda mfupi uliopita  Meneja Hafidh Saleh amesema hakukuwa na muda wa kusubiri hasa baada ya matokeo mabaya kwenye mchezo dhidi ya Prison hivyo benchi la ufudi liliona kuna haja ya kuwahi haraka mjini Morogoro kufanya matayarisho makubwa kwa ajili ya michezo hiyo miwili.

Mara moja tulihitaji mwamko mpya, baada ya kupoteza mchezo hakukuwa na sababu ya kubaia Mbeya, hivyo tuko safarini muda huu kuelekea Morogoro kufanya matayarisho makubwa kwa ajili ya michezo miwili,tunahitahi kurudhisha morali na utulvu kikosi kabala ya dakika 90 zijazo- Hafidh.

Akiendelea zaidi Meneja Hafidh alisema timu zote mbili ambo Yanga inakwenda kuzikabiri  kwa maana ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi na Raayon Sports kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho ni timu nzuri amabazo zzinahitaji kufanya maandalizi mazuri ya kutosha ili kuweza kuzishinda.

Tunacheza na timu nzuri,tunahitaji kujipanga na kufanya maandalizi mazuri kuweza kushinda, Mtibwa ni wazuri, Rayon ni wazuri zaidi na mashindano ya kimataifa ni muhimu  kwetu hivyo tunahitaji utulivu na kurudisha morali kikosini kueleka michezo hiyo.

Hafidh Saleh.

Comments

7
Elikunda Mlay 10:59 pm May 11, 2018

Nawatakia maandalizi mema na MUNGU awawezeshe kupata ushindi ktk hizi me hi zilizopo mbele ili kuleta moral kwa mashabiki na wadau wote wa Yanga.

yamasoft 5:14 pm May 12, 2018

Mbele daima, nyuma mwiko, Yanga tunahitaji umoja na mshikamano ili kuganya vema katika CAF confederation Cup, wachezaji na viongozi ni vema kushirikiana na kufanyia kazi changamoto na dosari zilizojitokeza ili kuamsha morali ya timu!

lawrence Mwasenga v 7:59 pm May 12, 2018

kila la kheri wakimataofa

Nazoro JM 4:19 pm May 13, 2018

Hakika uyasemayo yafanyiwe kazi, maana kinachotokea sasa ni FEDHEA kwetu sote wana YANGA viongozi hamna budi kutambua changamoto iko wapi maana tunakoelekea mi nahisi ni pabaya zaidi kama tutaruhusu kipigo kingine.VIVA YANGA “MBELE DAIMA NYUMA MWIKO”

official d.one 12:39 pm May 14, 2018

mashabik tunaendelea kuisapoti klabu yetu pendwa ya yanga na tunawatakia maandalizi mazuri ktk michezo inayofuata

furtdso linopv 7:19 am August 30, 2018

I like this site very much, Its a real nice post to read and obtain information. “What is called genius is the abundance of life and health.” by Henry David Thoreau.

http://www.furtdsolinopv.com/

zvodretiluret 11:12 am September 7, 2018

I like this website so much, saved to bookmarks.

http://www.zvodretiluret.com/