KUFUATIA uwepo wa ‘tetesi’  kutoka mitandao ya kijamii, kuwa Yanga Sc  imevunja mkataba na mshambuliaji Donald Ngoma,Katibu mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzanaia  Bara, Charles Boniface Mkwasa  amejitokeza na kutupilia mbali taarifa hizo  akisema ni uzushi usiokuwa na maana yoyote.

Akizungumza na yangasc.co.tz  muda mfupi uliopita Mkwasa amesema kuwa klabu iliandaa kamati ndogo ndani ya sekretarieti kufuatilia na kuchunguza mwenendo mzima wa majeraha na matibabu ya mshambuliaji huyo raia wa Zimbambwe kabla ya  kutoa maamuzi ya mwisho kulingana na taarifa ambayo ingepatikana.

Wote tunafahamu kuwa  mchezaji amekuwa nje kwa kipindi kirefu  kupisha majeraha aliyonayo,awali zilikewepo na taarifa nyingi kumhusu ambazo zimetulazimu kufikiria njia mbadala za kujua udani wa matatizo au majeraha yanayomuweka nje  kwa kipindi chote hicho ilihali anapaswa kutimiza majukumu yake uwanjani kama mchezaji.

Akiendelea zaidi Mkwasa aliweka wazi kuwa kamati ndogo iliyoundwa imekwisha kamilisha kazi yake na kinachosubiriwa sasa ni muda tu kwa ajili ya kutoa maamuzi ya mwisho.

Kilichobaki ni suala la muda tu,mengi yameshakamilishwa,uwepo wa mechi za  karibu karibu (zinazofuatana) kwenye mfululizo wa michezo ya ligi ndiyo kumechelewesha kufikiwa kwa hatua ya mwisho,tunahitaji kukutana na mchezaji kisha tutanganza maamuzi, kwa hiyo si kweli kwamba tayari tmevunja mkataba na Donald Ngoma kama ambavyo inavumishwa.

Ni vyema mashabiki wetu watulie na kusubiri taarifa rasmi ya klabu.

 

HAPA CHINI KAULI YA KOCHA NSAJIGWA KUELEKA MCHEZO WA KESHO

Comments

11
Mohamed 1:19 am February 10, 2018

Na vipi kuusu beki aliye (festo) sajiriwa baada ya majaribio kufuzu atuja muona tena katika timu na maelezo ya timu yupo kwao swala hili lipo vipi nalo

Omary kitale 7:55 am February 10, 2018

Safi Sana yanga

Zaniali 8:38 am February 10, 2018

Eemwenyezimungu jaalia timu yangu pendwa ipate ushindi leo

ghalib 9:40 am February 10, 2018

Habari yanga sc nafuatilia sana timu yetu iwapo uwanjani timu ni nzuri na baadhi ya wachezaji wanafanya vizuri sana kama Yondan ila timu ina upungufu wa viungo na straika wa mwisho apewe muda mwingi dogo mkomola,said ronaldo na kipa kinda kabwili

ghalib 9:49 am February 10, 2018

Habari kuelekea mechi za kimataifa na za ligi kuu nashauli viongozi kuafanya scouting ya kutosha nchi nzima mm naamini vipaji vipo mfano kuna siku nimeangalia mazoezi ya yimu ya mugabe fc ya sinza niligundua kipaji cha kipa wao mmoja simjui ila ana mwili mdogo but anasafiri vizuri golini pia wana straiker wao mmoja naye ni mwembamba ila anautulivu mzuri sana katika umaliziaji

Abdulzaza 9:56 am February 10, 2018

Message… *safi sana

Charles 3:07 pm February 11, 2018

Tupo pamoja

MROPE, J. 1:12 pm February 12, 2018

Timu yetu ya Yanga iko vizuri tu na yanayotokea ni mambo ya kimpira na ni changamoto za kufanyia kazi na si muda muafaka wa kulaumiana

MROPE, J. 1:26 pm February 12, 2018

Yote ni kheri tu.

mzee Henri 11:37 pm February 13, 2018

Nimekuwa nikifuatilia matibabu ya wachezaji wetu ambao kwa muda mrefu wapo nje,ninacho jiuliza ni kuwa kuna ugumu gani kwa klabu kuwapeleka wachezaji wetu hata hapo India kwa matibabu zaidi ? Angalia Azam na sasa Simba mbona wanapeleka wachezaji wao nje?

zvodret iluret 11:14 am September 7, 2018

You are my intake, I possess few web logs and sometimes run out from to post .

http://www.zvodretiluret.com/