MKUU wa idara ya habari na mawasiliano  ya  Yanga Sc, Dismas Ten, amesema  maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba  hapo kesho yamekamilika  kwa asilimia mia moja na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za mchezo wenyewe uwanjani.

Akizungumza na www.yangasc.co.tz  mapema  leo, Ten alisema kuwa, baada ya siku nane  na mazoezi na matayarisho kupitia kambi ya Morogoro, kikosi cha mabingwa mara 27 wa ligi kuu ya Tanzania Bara  kilisafiri siku ya jana na kufika salama  jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo.

Timu yetu  ilisafiri jana na kufika salama hapa Dar, mazoezi ya siku nane yamefanyika kwa umakini mkubwa  kwa upande wa timu na kwa upande wa uongozi maanadalizi yote muhimu yamekwisha fanyika na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za uwanjani – Ten 

Akiendelea zaidi, Mkuu huyo wa idara ya habari aliweka wazi kuwa  hakuna shaka yoyote kikosini juu ya hali za wachezaji, wote wako vizuri isipokuwa mshambuliaji Donald Ngoma ambaye bado yuko nje ya uwanja akiendelea kuuguza majeraha ya goti yanayomkabili.

Ni ngoma pekee bado yuko nje ya kikosi kwa majeraha, wachezaji wengine wako vizuri hivyo ni wasaa wa benchi la ufundi kuona nani wanaweza kumtumia kulingana na ‘game plan’ waliyokuwa nayo,kuhusu Chirwa nafasi ya kucheza mchezo ni kubwa na siyo kweli kwamba ana kadi tatu za manjano kama ambavyo inazungumzwa kwenye mitandao ya kijamii na sehemu zinginezo.

Katika hatua nyingine Kocha Zahera Mwinyi amesema  ameridhishwa na uwezo wa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Yanga,anachohitaji ni muda wa kukaa nao ili aendelee kuwajenga na kuwaimarisha zaidi tayari kwa michezo ya kimataifa.

Mara baada ya kukamilika kwa taratibu, kocha Mwinyi rasmi anatajia kuchukua majukumu ya kukinoa kukosi cha Yanga na kuna uwezekano mkubwa akanza kukaa kwenye bechi kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya USM Alger Mei 6 jijini Algels.

Download Hapa

KAMA HUKUPATA NAFASI YA KUIONA YANGA TV 2   TUMEKUWEKEA HAPA

Comments

3
zvodret iluret 10:29 am September 7, 2018

I’m still learning from you, as I’m improving myself. I certainly enjoy reading everything that is posted on your website.Keep the tips coming. I liked it!

http://www.zvodretiluret.com/

furtdsolinopv 6:45 pm September 11, 2018

I really appreciate this post. I have been looking everywhere for this! Thank goodness I found it on Bing. You have made my day! Thanks again!

http://www.furtdsolinopv.com/

best digital marketing institute in bangalore 11:56 pm October 22, 2018

Youre so cool! I dont suppose Ive read anything like this before. So nice to discover somebody by original thoughts on this subject. realy appreciation for starting this up. this web site are some things that is required over the internet, a person with some originality. beneficial work for bringing interesting things to the web!

http://commissionoverdrive.online