KOCHA Mkuu wa Yanga SC George Lwandamina amemuanzisha mlinda mlango kinda Ramadhani Kabwili kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa msimu huu dhidi ya St Louis United ya Shelisheli unaotarajia kuchezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Muda mfupi uliopita Lwandamina ameiambia yangasc.co.tz kuwa Kabwili amekuwa na wakati mzuri mazoezini na zaidi alicheza vyema kwenye michezo miwili ya ligi  kwenye uwanja wa Uhuru na Samora Iringa ambayo yote kikosi kiliibuka na ushindi,hivyo ameona kuna uhalali wa kumuanzisha katika mchezo huu namba 25 wa ligi ya mabingwa.

Kiwango chake kimeimarika,kwa muda sasa tumekuwa tukimjenga kama mchezaji mdogo ambaye anapaswa kujiamini ili kukitendea haki kipaji chake,huu ni wakati wake kudhihirisha alichojaaliwa na Mungu,atacheza mchezo leo na binafsi sina wasiwasi  juu ya uwezo wake.

Katika hatua nyingine Lwandamina amesema kuwa mlinda mlango namba moja Youthe Rostand ambaye amerejea kutoka majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Lipuli bado ataendelea kuwa kipa namba moja ingawa inambidi kufanya kazi ya ziada kuendelea  kujihakikishia  nafasi yake.

Ni mlinda mlango bora,wote tunafahamu amerejea kutoka majeraha,jambo muhimu kwake ni kufanya mazoezi kwa nguvu kuendelea kuweka kiwango chake kwenye ubora,bado tunaamini ni mlinda mlango chagua la kwanza.

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOCHEZA LEO DHIDI YA ST LOUIS KIMEPANGWA HIVI:

Comments

12
mwasenga 12:49 pm February 10, 2018

kikosi kiko vizuri tu, mungu atujalie

Ramadhani salim 1:27 pm February 10, 2018

Kikosikizuli tumuombe mungu tu na tujazane kwawingi uwanjan

Ally Mfaume 1:46 pm February 10, 2018

maamuzi sahii na ni wakati wako wako kabwili kumsaidia kocha kwa kufanya vizuri zaid

Gift Erick 2:25 pm February 10, 2018

Mungu ibariki Yanga

Egidius Mushubirwa 2:49 pm February 10, 2018

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.

john 3:21 pm February 10, 2018

safi.Komaa kabwili utusue

ChrisJr 7:48 pm February 10, 2018

Tanzania One wa Hapo Kesho

Agrey Samson 10:38 pm February 10, 2018

Message… *MUNGU IBARIKI YANGA, TUJAALIE USHINDI SIKU ZOTE*

Hamidun 12:23 am February 11, 2018

Good start for Rama, much effort more power.

MROPE, J. 1:19 pm February 12, 2018

Amesajiliwa Yanga ili aitumikie na ana kiwango bora

McNamara Cogan 6:12 pm February 12, 2018

Ni jambo zuri kumpatia nafasi kijana kuonesha kipaji chake siku za usoni ataisaidia timu yetu

engi muro 3:01 pm February 13, 2018

dogo namtabiria makubwa