MSHABULIJI nyota wa Yanga Sc, Ibrahim Ajib  amesema  hana sababu yoyote ya kugoma  kuichezea  timu yake kama  inavyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na www.yangasc.co.tz mapema leo Ajib amesema kuwa  hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuamua kubakia nyumbani  kuipigania  afya ya mke wake  alikuwa tayari kujifungua baada ya miezi 9 ya ujauzito ulikuwa na matatizo mengi kiafya.

Kuna wakati nilikuwa na hofu kubwa,juu ya maisha ya mke wangu, uja uzito wake toka awali ulikuwa na matatizo mengi, nashukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike,hilo ni jambo jema kwetu kama familia,ndugu na jamaa kwa ujumla.

Akiendelea zaidi  Ajib  aliweka wazi  kusikitishwa na maneno makali  anayotumiwa  na mashabiki kupitia  jumbe za simu wakimlaumu kwa kugoma kwenda kuichezea timu yake kwenye mchezo wa kombe la shirikisho.

Sina sababu ya kugoma,kucheza mpira ndiyo kazi yangu, hofu kubwa niliyokuwa nayo juu ya afya ya mke wangu kutokana na matatizo ya ujauzito aliokuwa nao hata kama ningeenda nadhani nisingeweza kucheza vizuri, kati yetu hakuna asiyejuwa juu ya matatizo yanayowakuta mama zetu.

Comments

4
Khalid 10:20 pm May 5, 2018

Kila la kheri

Phil 9:16 am May 16, 2018

This is good but the team need to be improved. Can we train Raphael to play number 9?

Phil 9:24 am May 16, 2018

All the best in your encounter with Rayon. Players should fight to make Yanga proud today

zvodret iluret 5:41 pm August 31, 2018

Some truly interesting information, well written and generally user friendly.

http://www.zvodretiluret.com/