IKICHEZA umakini mkubwa,Yanga sc imefanikiwa kuvuna ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji ya Songea kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Papy Kabamba Tshishimbi ndiyo alikuwa wa kwanza  kuifungia Yanga bao kufuatia mlinzi wa Majimaji kuunawa mpira uliokuwa umepigwa na Obrey Chirwa ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru adhabu ya penalti.

Kuingia kwa bao hilo kuliongeza harakati za mashabulizi kwa Yanga, na dakika kumi baada ya bao la kwanza Obrey Chirwa alifanikiwa kufunga bao la pili katika mchezo wa leo likiwa bao lake la 11 msimu huu kufuatia krosi ya Gadiel Michael.

Emmanuel Martin alihitimisha dakika 45 za kwanza kwa kufunga bao la tatu baada ya kufumua shuti kali akiwa umbali wa mita 30,hivyo hadi timu zote zinakwenda mapumziko Yanga ailikuwa mbele kwa bao 3-0.

Majimaji walikianza vyema kipindi cha pili na kufanikiwa kupata mkwaju wa Penalti kufuatia makosa ya walinzi wa Yanga na wageni hao kufanikiwa kupachika wavuni penati hiyo.Furaha ya timu hiyo kutoka Songea ilikoma kwenye dakika ya 54 baada ya Papy Kabamba kufunga bao la nne kwa Yanga lililohitimisha  dakika 90 za mchezo huo.

Mara baada ya mchezo kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa aliwashukuru wachezaji kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kupata ushindi ambao umeongeza nguvu ya kupata mafanikio zaidi kwenye michezo ijayo

Tumecheza vizuri,hongera kwa vijana wetu kwa namna walivyocheza na kutuhakikishia pointi tatu muhimu, limekuwa jambo jema sisi kushinda mchezo huu kwa sababu hii ni chachu kuelekea michezo ijayo, tunahitaji kuendelea  kushinda ili kutenegeneza mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wetu.

Yanga Sc  inataraji kuondoka nchini siku ya jumapili kuelekea Victoria  huko Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji St Louis iliyopangwa kuchezwa tarahe 21/2/2018.

 

Kama hukupata nafasi ya kuona mchezo huu, haya hapa magoli 3.

Comments

13
Salimuabou 7:32 pm February 14, 2018

Hongera Yanga, hongera wachezaji!
Kipindi cha pili nguvu ilipungua sana na timu ilishambuliwa..

mwasenga 7:58 pm February 14, 2018

safi wanajangwani Mungu amejalia ushindi tumepata ni suala la kushukuru

Hamza Kabisa 8:02 pm February 14, 2018

Daimba Mbele Nyuma Mwiko

benard 8:16 pm February 14, 2018

Kazi nzur vijana

Hamza Kabisa 8:18 pm February 14, 2018

#DaimaMbeleNyumaMwiko

Pastory JM 8:33 pm February 14, 2018

Yanga yangu…… Timu yangu

Benny killian 8:39 pm February 14, 2018

Safi kikubwa kujenga zaidi morality kila mchezo Ni kama fainali.
Bravo young africans sports club

Frank Fungo 8:46 pm February 14, 2018

Hongera sana pendwa.
Ombi langu kwa viongozi was Matawi pamoja na viongozi wa team ni kubuni njia ya kuongeza washabiki..team yetu siku hizi imepinguza sana washabiki sana inaweza kua kutokana na either aina ya Moira wetu was sasa au uhakika wa matokeo …lakini Mimi naomba wafanye yafuatayo:-
1.Club yaan uongozi kuanzisha bajeti ya matangazo yenye motisha za kwenye vyombo vya habari.
2.Club ianzishe kamati ya uamasishaji either kwa kuwatumia watu maaufu wenye mapenzi na Yanga.
3.Viongozi was Matawi kuanza kuamasisha watu kuanzia mitaani.
4.Kama VIP ile namba ya kuchangia team irudi pia mana tunaamini team ni ghalama kapa ilivyo ghalama kupata Furaha yeyote ile
#YangaYetuFurahaYetu.

Gilbert 11:26 pm February 14, 2018

Axante Vijana Kwa Kazi Nzuri Ya Leo Zaid Ni Kuongza Ngvu

Kembo 7:14 am February 15, 2018

The dream team

Musa 8:15 am February 15, 2018

We played very well yesterday. Hope we will shift the game pace to CL games. Keep it up Dar Young Africans

ChrisJr 9:53 am February 15, 2018

Hongera Yanga

zvodret iluret 9:19 pm August 28, 2018

This is the best weblog for anybody who desires to seek out out about this topic. You notice so much its virtually laborious to argue with you (not that I actually would want…HaHa). You undoubtedly put a brand new spin on a topic thats been written about for years. Nice stuff, simply nice!

http://www.zvodretiluret.com/