KIKOSI cha Yanga Sc  kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka Shelisheli tayari wa mchezo wa marejeano na wenyeji  St Louis Fc kwenye ligi ya mabingwa afrika mchezo ulipangwa  kuchezwa jumatano ijayo Stade Liete.

Muda mfupi  uliopita  Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten ameiambia  yangasc.co.tz kuwa  jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao 8 kutoka benchi la ufundi watasafiri asubuhi ya kesho  kupitia Nairobi tayari kwa mchezo huo muhimu  siku ya jumatano.

Maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika,timu imefanya mazoezi ya mwisho leo tayari kwa safari hiyo,kwenye kikosi nyota waliokuwa na majeraha ya muda mrefu kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu na Yohana  Mkomola wataendelea  kukosekana hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha, kucheza ugenini kuna changamoto zake lakini tumejiandaa vizuri kwa sababu tushacheza nje mara nyingi hivyo hakuna hofu kati yetu.

Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa, wachezaji  Thabani Kamusoko ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi pia ameondolewa kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate muda wa kujifua zaidi ili kurejesha makali yake, sambamba na  Obrey Chirwa ambaye naye  hayumo kwenye orodha ya wachezaji watakaosafiri kwa sababu ya maumivu ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majiamaji.

Ilikuwa asafiri  kueleka Shelisheli, lakini taarifa ya vipimo muda mfupi uliopita imelazimu benchi la ufundi kumuondoa kwa sababu bado hajawa ‘fit’ asilimia 100,anahitaji muda wa kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani,daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha aliyokuwa nayo,Chirwa ana maumivu ya misuli,hatakuwepo Shelisheli.

Orodha kamili ya wachezaji ambao safiri kuelekea Shelishelini kama Ifuatavyo:

Ramadhani Kabwili,Beno Kakolanya,Youthe Rostand,Hassan Kessy,Juma Abdul,Mwinyi Haji,Gadiel Michael,Nadir Haroub,Patto Ngonyani,Kelvin Yondani,Said Juma,Papy Tshishimbi,Pius Buswita,Raphael Daud,Yussuf Mhilu,Ibrahim Ajib,Said Mussa,Emmanuel Martin,Geoffrey Mwashiuya,Juma Mahadhi.

Comments

9
Ambrose Maestro 3:59 pm February 17, 2018

…daaa hawa majerudi wanaongezeka kila kukicha ee Mungu kuepusha na hili janga

Rochas Yotham 4:34 pm February 17, 2018

kwani chirwa ana tatizo gani jamani mbona hamjasema.mnatupa pressure mashabiki

Novatus Martine 6:38 pm February 17, 2018

Hawa majeruhi season hii yametuandama mno asee!!chamsingi viongozi wetu endeleeni kuwatia moyo wachezaji ambao wako fit ili morali yao iwe juu na Tuendelee kupata matokeo chanya

Yusufu msaliko 7:45 pm February 17, 2018

Ngoma na tambwe wanafaa kuvunjiwa mikataba yao

Omary kitale 8:37 pm February 17, 2018

Tujipange na kikosi kilichopo maana tulisajili wachezaji 25 ili waisaidie yanga

Khalidi A. Nyangasa 8:43 pm February 17, 2018

Kila la gheri dua nyingi tunawaombea.

Muta 11:51 pm February 17, 2018

Huyu bundi wa majeruhi sijui kwanini hataki kutoka juu ya paa!! kila la kheri wanajeshi wetu ushindi muhimu.

Elia lonje 7:40 am February 18, 2018

Naona tunaandamwa na majeruhi wengi madaktari wajitathmini upya kwanini wachezaji hawaponi

zvodretiluret 9:11 am August 28, 2018

I’m not that much of a online reader to be honest but your blogs really nice, keep it up! I’ll go ahead and bookmark your site to come back down the road. Cheers

http://www.zvodretiluret.com/