KIUNGO  Pius Buswita  leo asubuhi amefanya mazoezi na sambamba na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza. kufuatia nafuu ya maumivu ya kifundo cha mguu yaliyoibuka  baada ya mchezo wa ligi dhidi dhidi ya Njombe Mji jumanne iliyopita.

Mkuu wa kitengo cha utabibu cha Yanga sc, Dr Edward Bavu, amesema  Buswita alianza kulalamika. maumivu makali nyuma ya mguu wake na baada ya vipimo vya X-RAY waligundua tatizo ambalo lilihitaji mapumziko na matibabu ya haraka.

Tulimchukua hospital kwa vipimo zaidi,tuligundua tatizo kwenye kifundo cha mguu mara baada ya X-ray, matibabu ya haraka yalifanyika na hali yake kuimarika, leo amefanya mazoezi asubuhi amefanya mazoezi na anaonekana yuko safi, hivyo ni jukumu la wataalamu wa ufundi kuona kama wanaweza kumtumia kwenye mchezo wa kesho lakini kwetu sisi madaktari, yuko huru kucheza.

Buswita alikuwa na kiwango kizuri kwenye michezo miwili ya ligi, akifunga goli moja  dhidi ya Lipuli fc kwenye uwanja wa Samora, na kutoa pasi ya goli kwenye mchezo dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Comments

0